WhatsApp Image 2023-08-04 at 19.31.44

Waziri ahudhuria kikao cha kujadili Mikakati ya Ukusanyaji wa Kodi za ndani mwaka mpya wa fedha 2023/2024

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Mhe. Dkt Saada Mkuya Salum Leo Agosti 4, 2023 amehudhuria kikao cha kujadili Mikakati ya ukusanyaji wa Kodi za ndani Mwaka Mpya wa Fedha 2023/2024 katika Ukumbi wa Ofisi ndogo ya Hazina Jijini Dar es salaam.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Waziri wa Fedha wa Tanzania Dkt Mwigulu Lameck Nchemba, Waziri wa Tamisemi wa Tanzania Mhe. Angela Kairuki pamoja na Makamishna wa TRA na ZRA

Aidha, Dkt Mwigulu ameeleza kuwa kutokaa na maboresho ya mifumo ya kukusanyia Kodi Mwaka wa Fedha 2023/2024 Tanzania inatarajia kukusanya ShilingiTirioni 26.74

Nae, Dkt Saada Mkuya ameeleza kuwa Mamlaka ya Mapato Zanzibar itaendelea kushajihisha na kusimamia Wafanyabiashara kutumia mashine za elektroniki za kutolea risiti (VFMS) ili kudhibiti upotevu wa Mapato kwani Mwaka wa Fedha 2023/2024 ZRA inatarajia kukusanya Tsh Bilioni 520.64

Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Ofisi ya Rais Fedha na Mipango
Zanzibar

Tags: No tags

Comments are closed.