WhatsApp Image 2023-10-26 at 08.10.41

Dkt Saada amuwakilisha Mhe. Rais katika Uzinduzi wa Airpay Tanzania na PPP Portal

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango Mhe. Dkt Saada Mkuya Salum Leo Oktoba 25, 2023 amemuwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi katika Uzinduzi wa Airpay Tanzania pamoja na mfumo wa Public Private Partnership (PPP) katika Ukumbi wa Golden Tulip Mjini Zanzibar

Mhe. Saada Mkuya Kwa niaba ya Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi ameeleza kuwa zana ya Uchumi wa Buluu itafanya kazi vizuri kupitia mfumo wa Airpay kwani itarahisisha miamala ya kifedha Kwa njia za cashless pamoja na kuweza kutambua miamala ya kifedha inayofanywa na wafanyabiashara na wawekezaji wa sekta hiyo.

Mhe. Waziri Saada ameitaka Airpay Tanzania kufanya kazi Kwa karibu na Taasisi za SMZ kama ZRA ili kurahisha ukusanyaji wa Kodi Kwa njia za kieletroniki

Nae, Mkurugenzi Mkuu wa Airpay Mr Kunal Jhunjhunwala ameeleza kuwa lengo la teknolojia hii ni kurahisisha miamala ya kifedha na malipo na Kila mtu aweze kufikiwa na kutumia huduma hii

Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Serikali Mtandao Zanzibar Ndg Said Seif Said ameeleza kuwa Airpay Tanzania itasaidia Wananchi kupata huduma Kwa njia ya kidigitali pamoja na kuwarahisishia wawekezaji na wafanyabiashara kujisajili na kufanya malipo Kwa urahisi zaidi

Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango

Tags: No tags

Comments are closed.