Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe. Dkt Juma Malik Akil amesema uhai wa Bodi ya kwanza ya wakurugenzi ya ZIAAT imepata muelekeo mzuri kwa Nchi kutokana na wajumbe wake kufanya kazi kwa uweledi, uadilifu na utaalam kwa kuzingatia elimu na Sheria.
Dkt. juma Akil ameyasema hayo leo tarehe 03 Oktoba, 2026 katika Ukumbi wa Ofisi za ZURA wakati alipokuwa katika hafla ya kuiaga Bodi ya ZIAAT iliyomaliza muda wake wa miaka mitatu ya utendaji kazi
Mhe. Waziri amesema wajumbe wa Bodi hiyo ni wataalamu wa kiwango cha CPAs walio tukuka ambawo wamefanya kazi kwa viwango vya elimu, ubora na kufuata Sheria jambo ambalo imeifanya taasisi hiyo kuwa na mwazo mazuri na kuleta maendeleo kwa taaluma ya Uhasibu, Ukaguzi na Kodi
“kwa hakika mmefanya kaziI nzuri naamini kipindi kitachofuata watakao kuja wataendea vizuri kwani mmetoa muongozo mzuri utaosaidia masuala ya Fedha na Uhasibui,” alisema Mhe. Waziri wa Fedha Zanzibar
Dkt. Juma Akil aliishukuru Bodi hiyo na wajumbe wake kwa kusema amepata imani kubwa kuona dhamira ilioundiwa Bodi hiyo imefikiwa.
Nae, Mwenyekiti wa Bodi hiyo CPA Juma A Muhammed alisema kuwa bodi hiyo ilikuwa na wajumbe sita na ilikuwa na kamati tano ambazo ni kamati ya fedha na utawala, kamati ya Mitihani, kamati ya Nidhamu, kamati ya udhibiti wa ubora na kamati ya ukaguzi.
CPA Juma Amour alisema kazi za bodi hiyo ni pamoja na kutoa elimu kwa wahasibu na wakaguzi na washauri elekezi wa kodi Zanzibar pamoja na kufanya usajili kwa wanachama.
Mwenyekiti huyo alishukuru serikali kwa kufanya maamuzi makubwa kwa kujenga taasisi hiyo ambayo ina jukumu muhimu katika kuleta maendeleo na udhibiti wa rasilimali za Nchi
alisema katika kipindi cha miaka mitatu waliweza kujenga mifumo ya usimamizi wa udhibiti ubora wa taaluma, usajili wa wanachama, kutoa mitihaniI, kutoa mafunzo ya kitaaluma, usimamizi wa fedha.
Aidha, alisema kutokana na hayo Bodi hiyo imeweza kusajili wanachama 844.
Bodi ya wakurugenzi ya ZIAAT ilizinduliwa Novemba 4, 2023 na kumaliza muda wake Oktoba, 03 206.