

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Mhe. Dkt Saada Mkuya Salum Leo Agosti 28, 2023 amekutana na Ujumbe kutoka Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID), Ujumbe huo uneongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa USAID Tanzania Mr Craig Hart ambao walifika Ofisini Kwa Mhe. Waziri kujitambulisha
Dkt Saada Mkuya Salum ameutaka Uongozi wa USAID kuendelea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwa ni pamoja na kuisaidia SMZ katika vipaumbele vyake ambavyo ni elimu, afya, miundombinu, Uchumi wa Buluu, Nishati na kilimo cha kisasa na teknolojia
Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango
29 Agosti, 2023