








Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Mhe. Dkt Saada Mkuya Salum leo Sept 04, 2023 ameshiriki katika zoezi la utoaji zawadi Kwa washindi kumi (10) wa zoezi la Kila Mwezi la “Dai Risiti, Somba Zawadi” linaloendeshwa na Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA)
Zoezi hilo limefanyika katika viwanja vya Darajani, Mjini Zanzibar ambapo zawadi mbalimbali zimetolewa ikiwa ni pamoja na Simu, TV, Blenda na Redio Kwa washindi kumi wa Mwezi wa Agosti, 2023
Mhe. Waziri amewataka Wafanyabiashara kudai risiti za kieletroniki pindi wanaponunua bidhaa na kutoa taarifa Kwa Mamlaka ya Mapato Zanzibar Kwa Wafanyabiashara wanaokataa kutoa risiti za kieletroniki.
Nae, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar Ndg. Yussuf Juma Mwenda ameeleza kuwa zoezi hilo la utoaji zawadi Kwa wadai risiti bora ni miongoni mwa Mikakati ya kushajihisha Wananchi kudai risiti za kieletroniki pindi wanunuapo bidhaa
“LIPA KODI KWA MAENDELEO YA ZANZIBAR”
Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango
04 Sept, 2023