Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Mhe. Dkt Saada Mkuya Salum leo Julai 18, 2023 amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), tawi la Zanzibar
Hafla hiyo, imefanyika katika Ukumbi wa BOT Kinazini Mjini Zanzibar
Mhe. Waziri ameeleza kuwa lengo la ziara hiyo ni kutaka BOT kuzidi kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutokana na mabadiliko ya Kiuchumi Zanzibar
Aidha, Mhe. Waziri ameutaka Uongozi wa BOT kuendelea kutoa elimu ya fedha Kwa Umma ili Wananchi waendane na mabadiliko ya teknolojia na mifumo ya fedha
Dkt Saada Mkuya Salum ameendelea kusisitiza Uongozi wa BOT kushirikiana na Serikali katika kuboresha mifumo ya fedha ili kuongeza ufanisi wa ukusanyaji mapato ya Serikali
Nae, Mkurugenzi wa BOT (Tawi la Zanzibar) Dkt Camilius Kombe ameeleza kuwa BOT, tawi la Zanzibar imefanikiwa kupunguza mfumuko wa bei Zanzibar, ambapo Kwa Sasa ni 6.5,%, Burundi mfumuko wa bei 28%, na Rwanda ni 20%, hivyo BOT imefanikiwa Kwa kiasi kikubwa kupunguza mfumuko wa bei.
Dkt Kombe ameendelea kueleza kuwa Sekta ya Fedha Zanzibar imeimarika Kwa kiasi kikubwa kwani Kwa sasa Zanzibar Kuna taasisi za Fedha (Mabenki) 14, Matawi 33, ATM 70 na Mawakala 816
Dkt Camilius amemshukuru Mhe. Waziri Kwa kufanya ziara ya BOT na kumuahidi Mhe. Waziri kuwa maelekezo yote watayafanyia kazi pamoja na kutoa elimu ya fedha Kwa Umma



Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango
18 Julai, 2023