Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

wizara ya Fedha na Mipango

Habari & Matukio

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Juma Malik Akil, amewataka wanafunzi wa Kada ya udaktari kuanza kujenga uwezo wa uongozi, ubunifu na utumishi wa jamii tangu wakiwa vyuoni.

Dkt. Akil ameyasema hayo alipokuwa akifungua Mkutano wa 18 wa Kimataifa wa Kisayansi na Mkutano Mkuu wa 16 wa TAMSA, unaofanyika Zanzibar.

Amesema uwekezaji katika afya haupaswi kuishia kwenye hospitali, vifaa na teknolojia, bali unapaswa pia kuzingatia rasilimali watu.

Amesisitiza kuwa wataalamu wenye ujuzi, maadili na kujituma ni muhimu katika kuboresha huduma za afya.

Aidha, amewataka madaktari vijana kutumia ubunifu na teknolojia kutafuta suluhisho na changamoto za afya.

Aidha amewata madaktari hao kutoa huduma bora zitakazowafikia wananchi wote, wakiwemo wanaoishi vijijini na makundi yaliyo katika mazingira magumu.

Mkutano huo wa TAMSA unafanyika Zanzibar kuanzia Septemba 30 hadi Oktoba 3, 2026, ukiwakutanisha wanafunzi wa tiba na wadau mbalimbali kwa ajili ya mijadala ya kisayansi, uongozi na masuala ya afya.

Scroll to Top