Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Ndg. Aboud H. Mwinyi leo Oktoba 19, 2023 amefungua warsha ya siku mbili kuhusu mafanikio na changamoto za programu zinazodhaminiwa na UNICEF katika Ukumbi wa Golden Tulip Mjini Zanzibar
Ndg. Aboud ameeleza kuwa, semina hii ni muhimu sana kwani sekta husika ikiwa ni pamoja na maji, afya, elimu pamoja na ustawi wa jamii zimefanikiwa Kwa kiasi kikubwa Kwa mchango wa UNICEF katika kuboresha sekta hizo.
Aidha, Ndg. Aboud amewataka washiriki wa warsha hiyo kupitia Kwa umakini changamoto zilizojitokeza Mwaka uliopita ili zisiwe kikwazo Kwa Mwaka mpya wa utekelezaji wa programu hizo.
Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango


