WhatsApp Image 2023-10-27 at 14.39.41

Mhe: Waziri Dkt. Saada Mkuya akutana na Uongozi wa ASA Microfinance Limited

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -Fedha na Mipango Mhe. Dkt Saada Mkuya Salum leo Oktoba 26, 2023 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kifedha (ASA Microfinance Limited) Bibi Karin A. M.Kersten) ambae ameambatana na wajumbe mbalimbali akiwemo Mkurugenzi wa ASA Kwa upande wa Tanzania Ndg Muhammad Shah Newaj

Bibi Kersten ameeleza kuwa Uongozi wa ASA umefika Ofisini Kwa Mhe. Waziri Kwa lengo la kujitambulisha na kueleza kuwa Kwa upande wa Tanzania Ofisi za ASA Microfinance Limited zinapatikana Kinondoni, Jijini Dar es Salaam

Aidha, Bibi Kersten ameendelea kueleza kuwa Kwa upande wa Zanzibar Ofisi za ASA zinapatikana Maungani, Wilaya ya Magharib ‘B’ Mkoa wa Mjini Magharib

Dkt Saada Mkuya ameushukuru Uongozi wa ASA Kwa kufungua tawi lake Kwa upande wa Zanzibar kwani itakuwa ni fursa Kwa wajasiriamali wa sekta mbalimbali hasa sekta ya Uchumi wa Buluu kwani ndio kipaumbele Cha kuwakomboa Wazanzibari wengi ambao wanajishhhulisha na kilimo Cha mwani na uvuvi wa kawaida.

Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango

Tags: No tags

Comments are closed.