WhatsApp Image 2023-05-19 at 1.56.12 PM (2)

Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango imeanza zoezi la kuhakiki wazee ambao wanapokea pencheni jamii.

Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango kupitia Ofisi ya Mhasibu Mkuu wa Serikali imeanza zoezi la kuhakiki wazee ambao wanapokea pencheni jamii.

Zoezi hilo linafanyika kutokana na ongezeko la pencheni jamii iliyotangazwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango wanashirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na watototo pamoja na PBZ kwa ajili ya kuwafungulia akaunti wazee hao na malipo hayo yataanzia mwaka wa fedha unaoanzia July 2023.

Zoezi hilo limefanyika katika Wilaya ya Magharibi B, katika skuli ya Fuoni.

Imeandaliwa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango.

Tags: No tags

Comments are closed.