Mhe. Waziri amefanya ziara ya kikazi Bandarini Mjini Zanzibar.

Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe. Jamal Kassim Ali amefanya ziara ya kikazi Bandarini Mjini Zanzibar na kuonana na watendaji katika Taasisi ya TRA, Mheshimiwa amegundua uzembe wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali uliofanywa n wafanyakazi wa TRA wa Bandarini kwa kuitoa gari nje ya bandari kinyume na taratibu za sheria ya Zanzibar.

Hali hiyo ilimkasirisha Mhe. Jamal na kutoa maagizo mawili kwa Naibu Kamishna wa TRA juu ya wafanyakazi wa TRA waliopo Bandarini pamoja na Agent aliehusika kuitoa gari hiyo.

Agizo:

  1. Mhe. Jamal Kassim alizitaka taasisi zinazo husika kufanya uchunguzi wa kina na ikibainika wafanyakazi hao wamechangia kuikosesha Serikali Mapato kwa kuitoa gari nje bila kumalizika kwa taratibu wachukuliwe hatua ikiwa ni kusimamishwa kazi na kupelekwa Mahakamani ili sheria ipitishe mkondo wake na Agent anaehusika pia achukuliwe hatua za kisheria. Aidha, Mhe. Waziri alisisitiza kusema haiwezekani kwa gari kutolewa usiku wakati Bandarini pana walinzi na Milango imara Bandarini hapo.
  2. Mhe. Waziri ametoa wiki na alimuamuru Naibu Kamishna TRA kulirudisha gari hilo haraka iwezekanavyo ili lifuate taratibu za malipo ya kodi na kama kuna adhabu ya malipo apewe ili iwefundisho kwa wengine. Mhe Jamal amesema kodi ni muhimu kwa Maendeleo ya Nchi kwani zinatumika katika nyaja mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya, Maji na Kujenga Miundombinu imara ya Nchi. Mheshimiwa Jamali katika Ziara yake hiyo aliongozana na Waziri Mwenzake wa Mawasiliano.