Mhe. Waziri akutana na kufanya maongezi na Benki ya Dunia(World Bank)

Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe. Jamal Kassim amesema Serikali kupitia Bank ya Dunia (World Bank) ambayo inatufadhili kuitekeleza Miradi 13 ya Maendeleo hapa nchini. Nd. Amandeep Virk wa Kampuni ya ICT alifanya utafiti wa miradi mbali mbali ya Uwekezaji wa sekta binafsi ili kuimarisha wawekezaji binafsi kuja kuekeza nchini.

 Mhe. Jamali amesema Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi imeweka mikakati mizuri ya kuitatekeleza miradi hiyo 13. Miradi hiyo ikiwemo Masoko 4 yatajengwa Unguja na Pemba 1 Kituo vya paking 1, vituo vya daladala 2 kwa unguja na vituo basi 3 kwa Pemba, dahalia ya wanafunzi SUZA ya Tunguu 1, kituo cha kusarifu takataka 1 kitajengwa mlilile Matemwe, umeme wa sola katika vituo vya maji zawa na kituo cha kimataifa cha biashara nyamanzi 1,

Aidha, Mhe.Jamal aliyasema hayo Katika warsha ya siku mmoja wakati wa kufunga warsha hiyo iliyoandaliwa na PPP iliyowajumuisha sekta binafsi na banki ili kuweza kuipitia mradi mmoja mmoja kwa kuijadili gharama za Miradi hiyo na aina za Uekezaji wake.

Aidha, Mhe. Jamal amezitaka sekta binafsi kushirikiana na Serikali katika kutekeleza Miradi hiyo ambayo itabadilisha haiba ya mji wa Zanzibar na kupelekea Ukuwaji mkuwa wa Uchumi na Kupunguza Umasikini ndani ya nchi.  Mhe.  Waziri amesema miradi hiyo itakapo tekelezwa itaibua ajira nyingi kwa wananchi wetu na Miradi hiyo inatarajiwa kuanza kutekelezwa mwaka huu wa Fedha.