About Us

Afisi ya Rais Fedha na Mipango imeanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 kifungu namba 104 na Sheria ya Tume ya Mipango namba 3 ya mwaka 2012 yenye jukumu la kusimamia upatikanaji na matumizi bora ya Fedha za Serikali pamoja na kuandaa Mipango madhubuti ya maendeleo ya nchi.