BADEA yaendelea kuisaida Zanzibar kwa miradi ya maendeleo

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefanya majadiliano na Mkurugenzi Mtendaji wa BADEA ili kuona Miradi mbalimbali iliyomalizika na inayoendelea ambayo inafadhiliwa na BADEA. Ujio wa Mkurugezi Mtendaji na Ujumbe wake ni kuja kuangalia Miradi hiyo. Jumla ya fedha zinazotarajiwa kutumika katika Miradi inayoendelea ni USD 15 Millioni. BADEA itatoa 13.5 na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni 1.5 Mhe. Jamal amesema miradi ya kimaendeleo inayo endelea atahakikisha inatekelezwa na kumalizwa kwa wakati husika. Jumla ya miradi inayoendelea ni mi nne. 1. Matengenezo ya hospital ya Mnazi Mmoja. 2. Matengenezo ya barabara ya Wete – Chake kwa awamu ya pili yenye ukubwa 22.2 KM. 3. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali inatarajia kujenga skuli tatu. Mbili zitajengwa Unguja na Mmoja itajengwa  Pemba. 4. ZECO kufanya tafiti ambazo zitasaidia kusambaza umeme wa KV132. Mhe. Jamal na Mkurugenzi Mtendaji Dr.Sidi Ould Tah wameweza kujadili mambo mbali mbali ikiwemo Mashirikiano katika sekta za Kimaendeleo katika mpango wa miaka mitano pamoja na suala la Uchumi wa Blue, kuona jinsi BADEA watakavyo saidia kuanzia kujenga miundo mbinu wezeshi katika sekta hiyo na kuweza kuvijengea uwezo vyuo vyetu katika kuhakikisha vinazalisha wataalamu ambao watasaidia sekta ya Uchumi wa Blue. Majadiliano hayo yamefanyika katika Ofisi ya Rais Fedha na Mipango.

Serikali Mapinduzi ya Zanzibar kusaini mkataba na balozi wa Sweden

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetiliana Saini na Serikali ya Sweden,  Jumla ya dola millioni 5.4…

Mhe. Rais wa Zanzibar afanya mazungumzo na Ujumbe wa BADEA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Mwinyi amekutana na Kufanya mazungumzo na Ujumbe wa BADEA. Ujumbe huo umewasili Ikulu wakiwa na mwenyeji wao Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango, Mhe. Jamal Kassim Ali na Mkurugenzi Mtendaji wa BADEA Dr. Sidi Ould Tah

Mhe. Waziri kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Wizara ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kiuchumi ya Ujerumani

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMEDHAMIRIA KUWALETEA MAENDELEO YA HARAKA WANANCHI WAKE KUPITIA SEKTA MBALI MBALI.…

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango akutana na wahasibu katika ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Dk. Juma Malik Akili, amesema bado kasi ya…