Mheshimiwa Dkt. Saada Mkuya Salum ametembelea Taasisi ya Shirika la Bima la Zanzibar

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Mheshimiwa Dkt. Saada Mkuya Salum ametembelea Taasisi…

Mhe. Dkt. Saada Mkuya ameutaka Uongozi na Wafanyakazi wa ZSSF

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Saada Mkuya ameutaka Uongozi na Wafanyakazi wa ZSSF kutimiza wajibu wao na kutoa huduma bora kwa wanachama wao Pamoja na kushughulikia vyema mafao ya Uzazi kwa wanachama wanaostahiki mafao hayo. Mhe. Waziri ameyasema hayo leo alipotembelea taasisi hiyo kwa lengo la kujitambulisha, amewahimiza wafanyakazi wa ZSSF kuitumia fursa iliyopo kwani ZSSF ni mfuko pekee unaochangiwa na wanachama ambao ni wafanyakazi wa Serikali Pamoja na wafanyakazi wa Taasisi binafsi ili mfuko uweze kufikia malengo yaliyokusudiwa na Serikali. Aidha, Waziri Dkt. Saada amewataka watendaji hao kuwa wabunifu zaid katika kufanya kazi zao ili kufanya kazi kwa ufanisi zaid. Mhe. Waziri ameiagiza ZSSF kuhakikisha kila muekezaji anawasajili wafanyakazi wake ZSSF na kuwaletea michango ya wafanyakazi hao kwenye mfuko huo. Pia Mheshimiwa Dkt. Saada aliiagiza ZSSF kuandaa miundombinu Madhubuti ya kupokea wanachama wapya hususan kwa upande wa Pemba, kwani mkakati wa Serikali ni kuimarisha kuwekezaji zaidi kwa Pemba na kuhakikisha muda wowote Mfuko unaweza kulipa mafao ya wanachama wanaostaafu na kutoa pencheni kwa wakati uliopangwa kisheria. Mheshimiwa Dkt. Saada amesajiliwa hapo hapo kuwa mwanachama wa mfuko huo na kukabidhiwa kadi ya uanachama hapo hapo. Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi Bi Khadija Shamte amesema wamepokea yale yote waliyoagizwa na Mheshimiwa Waziri na watayafanyia kazi kwa manufaa ya Mfuko, Na kusema ZSSF imeanzisha uwekezaji wa Miradi mipya mbalimbali na inatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Serikali imeandaa mkutano wa majadiliano na washirika wa maendeleo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Mheshimiwa Jamal Kassim Ali, amefunga Mkutano wa…