Mhe. Waziri akutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia (WB).

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, Fedha na Mipango,Mhe. Jamal Kassim Ali, leo amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia (WB) kanda ya Afrika group 1, Dk. Taufila Nyamadzabo, ofisini kwake Vuga. Mhe. Jamal ameipongeza Benki hiyo kwa misaada ikiwemo mikopo na ruzuku mikopo inayoipatia Zanzibar kwani imechangia kuimarisha ustawi bora na maendeleo Nchini. Mhe. Jamal amesema miradi mikubwa miwili nayo ni BIG-Z imetengewa Dola Milioni 150 na ZESTA imetengewa Dola Milioni 142, Miradi hiyo iliyoidhinishwa na Benki ya Dunia itaanza hivi karibuni na itachochea kwa kasi kubwa ukuwaji wa Uchumi Pamoja na maendeleo ya Zanzibar na watu wake. kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia (WB) kanda ya Afrika Group 1 dkt. Taufila Nyamadzabo, amesema Benki ya Dunia itasaidia Zanzibar katika miradi mbali mbali ya kimkakati ikiwemo eneo la Uchumi wa Buluu. Pia Dkt. Taufila Nyamadzabo, amesema Benki ya Dunia iko tayari  kusaidia ushiriki wa sekta binafsi katika Maendeleo. Aidha dkt. Taufila amesema kuwa sekta ya elimu na Afya ni sekta muhimu katika Maendeleo hivyo wako tayari kushirikiana na Serikali iweze kufikia malengo yake  iliyojiwekea.

Mhe. Waziri aeleza dhamira ya Kukusanya Mapato kwa mfumo mpya wa kielektroniki

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe. Jamal Kassim amesema Serikali inakadiriya kukusanya…

MAREKANI YAVUTIWA NA MAENDELEO YA ZANZIBAR.

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, Fedha na Mipango, Mhe. Jamal Kassim Ali, ameeleza kuwa Serikali…

Ufunguzi wa Jengo la PBZ Business Center.

Ufunguzi wa Jengo la PBZ Business Centres. Jengo limefunguliwa na Makamo wa kwanza wa Rais wa…

Ufunguzi wa Jengo la Hifadhi Building Tibirinzi ChakeChake Pemba

Ufunguzi wa Jengo la Hifadhi Building Tibirinzi ChakeChake Pemba

Mhe. Waziri azungumza na Wakaguzi wa ndani.

Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mheshimiwa Jamal Kassim Ali amesema Serikali haitomvumilia…

Mhe. Waziri akutana na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia.

Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mheshimiwa Jamal Kassim Ali amekutana na Balozi…

Mhe. Waziri afanya mkutano na wafanya Biashara tofauti katika ukumbi wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB).

Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe. Jamal Kassim Ali ameahidi kuboresha Mazingira…

Mhe. Waziri akutana na Viongozi mbalimbali wa kampuni za Bima Wizarani kwake – Zanzibar

Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe. Jamali Kassim Ali amekutana na Viongozi…

Mhe. Waziri akutana na kufanya maongezi na Benki ya Dunia(World Bank)

Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe. Jamal Kassim amesema Serikali kupitia Bank…