Fiscal Policy and Finance

KAZI KUU ZA IDARA

Kuanzisha, kufuatilia na kutathmini Misingi na Taratibu Zinazohusu Masuala ya Sera za Kodi, Sekta ya Fedha na Mapato yatokanayo na Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asili ili kuongeza uhamasishaji wa Rasilimali za Ndani na kuhamasisha Uwekezaji na Akiba.

Kushiriki katika Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa kuhusuiana na Kodi, Maendeleo ya Sekta ya Fedha na Mapato yatokanayo na Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asili.

Idara imeundwa na divisheni 3, ambazo ni Divisheni ya Sera za Kodi, Divisheni ya Sekta ya Fedha na Divisheni ya Sera za Mapato yatokanayo na Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asili.

DIVISHENI YA SERA ZA KODI

Lengo kuu la kuanzisha Divisheni hii ni kukuza sera za kodi na kuchambua athari za sera kodi kwenye uchumi na kuhakikisha mifumo ya kodi inakuwa bora, yenye ufanisi, usawa, haki na rahisi kueleweka na kutekelezeka.

Divisheni hii pia itawajibika kwa ufuatiliaji wa ukusanyaji wa mapato na usimamizi wake na pia kukadiria athari za mapato kutokana na mikakati ya hatua mbalimbali za kuimarisha mapato na kuhakikisha hali nzuri na imara ya kodi ndani ya uchumi. Divisheni hii ina sehemu tatu; Sehemu ya Sera ya Usimamizi wa Mapato, Sehemu ya Misamaha ya kodi na Sehemu ya Ujumuishaji wa kodi za Kikanda na Kimataifa; ambao kazi zao ni kama ifuatavyo;

KITENGO CHA USIMAMIZI WA SERA ZA MAPATO

Kufuatilia na kushauri Serikali juu ya usimamizi wa mapato yatokanayo na Kodi na mapato yasiyokuwa ya kodikwa Taasisi zinakusanya mapato na kupendekeza hatua za kukabiliana na hatua za kukwepa kodi na ukwepaji wa kodi.

Kufanya uchambuzi wa mapato na kufanya makadirio ya mapato yatokanayo na kodi na yasiyokuwa ya kodi katika kuhakikisha utulivu wa sera za kodi na matumizi.

Kushauri Serikali juu ya Ugawanyaji wa Fedha pamoja na uhusiano kati ya Serikali kuu na Mamlaka ya Serikali za Mitaa .

KITENGO CHA USIMAMIZI WA MISAMAHA YA KODI

Kushauri Serikali juu ya muundo, utekelezaji na usimamizi wa matumizi mabaya ya misamaha ya kodi (misamaha ya kodi na Unafuu wa Kodi) kufikia malengo ya kisera kwa maendeleo ya uchumi.

Kushauri Serikali juu ya sheria za kifedha za kuaminika (kama sheria za deni na sheria za matumizi), pamoja na uchambuzi wa uendelevu wa deni, kudhibiti kukopa na kuhakikisha kuwa serikali inaweza kulipa deni lake wakati wowote kutokana na mapato.

KITENGO CHA USIMAMIZI WA SERA ZA UTANGANISHO WA KODI ZA KIKANDA NA KIMATAIFA

Kushiriki na kuishauri Serikali katika ujumuishaji wa kikanda kama vile EAC, SADC, COMESA kwenye maswala ya Sera za Kodi.

Kushauri Serikali katika kuandaa mfumo wa Sera ya mkataba wa kodi na mkataba wa mfano na kushiriki mazungumzo ya makubaliano ya utozaji wa Kodi ya mapato (Mikataba ya kuondoa utozaji kodi mara mbili).

Kushauri juu ya matumizi ya sheria za kodi kwa miamala na biashara za kimataifa.

DIVISHENI YA SERA ZA FEDHA

Lengo kuu la divisheni hii ni kutunga na kufuatilia sera za fedha zitakazoendana na malengo ya uchumi, ushauri kuhusu masuala ya fedha za umma na sekta nyingine za fedha, kama vile benki, sekta ndogo ya fedha, mifuko ya pensheni, makampuni ya bima na masoko ya mitaji.

Kama inavyotakiwa chini ya uthabiti wa kifedha, divisheni hii itahakikisha Sekta za Fedha zinadhibitiwa na kusimamiwa ipasavyo ili kuchangia katika kupunguza umaskini hasa kwa kuongeza upatikanaji na matumizi ya huduma za kifedha na kuunda sekta ya fedha iliyoimara na shirikishi kupitia mageuzi ya lazima ya kifedha. Divisheni hii inajumuisha sehemu tatu; Sehemu ya Kitengo cha Sekta ya Benki, Kitengo cha Sekta zisizo za Kibenki na Kitengo cha Sekta Ndogo ya Fedha ambazo kazi zake ni kama ifuatavyo;

KITENGO CHA SEKTA YA BENKI

Kuimarisha, kusimamia na kufuatilia mchango wa sekta ya benki katika maendeleo ya kiuchumi

Kuishauri serikali kuhusu njia madhubuti za kuzuia matumizi mabaya ya mfumo wa fedha, uhalifu wa kifedha pamoja na utakatishaji fedha.

Kushiriki na kutoa ushauri juu ya jukwaa la kitaifa na kimataifa kuhusu maendeleo ya sekta ya benki.

KITENGO CHA SEKTA ZISIZO ZA KIBENKI

Kuimarisha, kusimamia na kufuatilia mchango wa sekta ya Hifadhi ya Jamii, Sekta ya Bima na Masoko ya Mitaji katika maendeleo ya kiuchumi.

Kutoa hatua za kiufundi ili kuboresha uhimilivu wa kifedha na sekta isiyo ya benki.

Kuratibu taratibu za utoaji wa deni na soko la mitaji kwa ajili ya shughuli za biashara na uwekezaji wa muda mrefu.

KITENGO CHA SEKTA NDOGO YA FEDHA

Kuunda uratibu, udhibiti na usimamizi madhubuti wa sekta ndogo ya fedha.

Kukuza utafiti, ubunifu na maendeleo ya bidhaa katika sekta ndogo ya fedha inayohusishwa na ulinzi thabiti wa watumiaji ili kuhakikisha ukuaji wa uchumi, ajira na kupunguza umaskini.

Kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa katika sekta ndogo ya fedha

DIVISHENI YA SERA ZA MAPATO YATOKANAYO NA UTAFUTAJI NA UCHIMBAJI WA MAFUTA NA GESI ASILI (PETROLEUM REVENUE POLICY DIVISION)

Lengo kuu la divisheni hii ni kuendeleza na kusimamia Sera za Mapato yatokanayo na Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asili ambazo zinakwenda sambamba na ukuaji wa uchumi na kutathmini,kuchambua na kukadiria Mapato yatokanayo na Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asili.

Divisheni hii imegawika katika sehemu kuu mbili; Kitengo cha Usimamizi wa Mapato yatokanayo na Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asili (Petroleum Revenue Management Section);na Kitengo cha Usimamizi wa Sera za Mapato yatokanayo na Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asili (Petroleum Revenue Policy Section).

KITENGO CHA USIMAMIZI WA MAPATO YATOKANAYO NA UTAFUTAJI NA UCHIMBAJI WA MAFUTA NA GESI ASILI

Kufanya Uchambuzi wa Mapato yatokanayo na Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asili

Kufanya makadirio ya mapato yatokanayo na Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asili

Kusimamia na Kufatilia mapato yatokanayo na Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta naGesi Asili

KITENGO CHA USIMAMIZI WA SERA ZA MAPATO YATOKANAYO NA UTAFUTAJI NA UCHIMBAJI WA MAFUTA NA GESI ASILI

Kusimamia na Kupendekeza Sera za Mapato yatokanayo na Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asili

Kupendekeza Miongozo ya Fedha juu ya Usimamizi wa Mapato na Matumizi yatokanayo na Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asili; na

Kupendekeza Wigo wa Kutozea Kodi kwa Makampuni ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asili