Mh. Waziri akutana na kufanya mazungumzo na muakilishi wa Shirika la Umoja wa Kimataifa UNCDF

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Mushemiwa Jamal Kassim(MBM)) leo amekutana na kufanya mazungumzo na Muwakilishi mkaazi wa Shirika la Umoja wa Kimataifa UNCDF , shirika linaloshughulikia masuala ya uwekezaji (mitaji) kujadili ushirikiano ya kuisaidia Zanzibar katika kuimarisha utendaji kazi wa utoaji wa huduma kwa Mamlaka ya Maji, Shirika Umeme na Ujenzi wa vituo vya Dalala Zanzibar.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika leo katika ofisi ndogo za SMZ zilizopo jijini Dar es Salaam waziri alisema lengo la mazungumzo hayo ni kuweka mikakati ya kushirikiana katika kutekeleza miradi mbalimbali ijnayotekelezwa na Hamlashauri na manispaa.

Alisema katika mazungumzo wamejadili namna ya kuzijengea uwezo manispaa, halmashauri Zanzibar ili waweze kutekeleza miradi mikubwa ya Masoko na Stendi za Mabasi.

Alisema Shirika hilo limekuwa likisaidia halmashauri mbalimbali nchini Tanzania katika kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo , hivyo wanataka kutumia fursa hiyo kushirikiana nao ili waweze kutekeleza miradi mikubwa Zanzibar.

“Tumeona tuna fursa ya kushirikiana nao kuendeleza miradi yetu ambayo tumeiweka katika bajeti yetu, tunashukuru wametupokea na ahadi waliyotupa sasa tutaenda kufanya kazi pamoja ili kuhakikisha miaradi ya mikubwa ya stendi ya mabasi, ujenzi wa masoko unaenda kuanza” alisema.

Alisema suala lingine ambalo wamelijadili ni uboreshaji wa miundombini katika sekta ya maji , kuzuia upotevu wa maji, na kuboresha ukusanyaji wa mapato ya maji.

“Hili ni eneo muhimu, litahusisha kuboresha miundombinu ya maji pamoja na kuweka mifumo mizuri itakayodhibidi upotevu wa maji” alisema.

Alisema kwa sasa mamlaka ya maji ya Zanzibar Zawa inakabiliwa na changamoto ya mapato kwani mapato yake mengi yanapotea kutokana na kutokuwa na mifumo mizuri ya kukusanya mapato ya maji.

Ameeleza suala lingine kuwa ni kuwajengea mazingira bora wajasiraiamali, , kuwajengea uwezo kwa kuwatafutia mitaji, kuwatafutia masoko na kuwapa elimu ya biashara ili waendelee kuwa kiungo mihimu katika kukuza uchumi.

“Wajasiriamali ni sehemu muhimu katika uchumi wa nchi yetu kwasababu wao ndio wanaofanya mzunguko wa fedha, wenzetu hawa tumezungumza nao, tunataka kuja na mfumo utakaorahisisha upatikanaji wa fedha , elimu na masoko” anaeleza.

Aidha alisema Afisi ya Rais Fedha na Mipango imejipanga kuhakikisha inatimiza malengo ambayo serikali imejiwekea. Pia Waziri Jamali amesema wamekubaliana baada ya wiki mbili wamepanga kukutana ili kufanya makubaliano na Shirika hilo ya kusaidia kutekeleza miradi hiyo mikubwa ya maendeleo.

Nae Ndugu Peter Malika amesisitiza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kukutana baada ya mazungumnzo hayo ya awali na wanatariajia kukutana baada ya wiki mbili na kufanya amzungumzo ya kutekeleza miradi mikubwa ya inayogusa maisha ya wananchi kama maji, ujenzi wa vituo vya Dalala na umeme.

“Tunaangalia miradi ya uwekezaji Zanzibar , miradi ya serikali, mashirika , miradi ya halmashauri hasa miradi ya kusambaza maji, umeme na ile unayowagusa wananchi “ alisema.