Mhe. Dkt Saada Mkuya Salum 2 amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Jumuiya ya Kimataifa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Mhe. Dkt Saada Mkuya Salum Leo Juni 16, 2022 amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Jumuiya ya Kimataifa inayojihusisha na Mifumo bora ya utoaji wa huduma za Kijamii hususan huduna ya afya. Jumuiya hiyo inatambulika Kwa jina la (PharmAccess Foundation) 
Uongozi wa PharmAccess Foundation ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Dkt. Nicole Spieker wamezungumzia juu ya namna bora ya kuisaidia Zanzibar katika Mifumo bora ya utoaji wa huduma ya Afya Kwa Wazanzibari wote.
Dkt. Nicole ameeleza kuwa PharmAccess Foundation wako tayari kuisaidia Zanzibar katika utengenezaji wa Mifumo bora ya Bima ya Afya (Zanzibar Health Insurance Scheme) 
Mhe. Dkt.Saada Mkuya ameiomba Jumuiya hiyo ipanue wigo zaidi katika kuisaidia Zanzibar kwenye  maeneo mengine kama upatikanaji wa maji safi na salama.
Dkt.Nicole ameeleza kuwa PharmAccess Foundation haijaanza Leo kuisaidia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, hivyo wapo tayari kujikita kuisaidia Zanzibar katika maeneo ya Afya na huduma nyengine za Kijamii.