Mhe. Jamal Kassim Ali afanya mazungumzo na Ujumbe wa Shirika la Ufadhili wa Misaada ya Fedha kutoka(UK FINANCE EXPORT)

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  imewakikishia  wananchi kuendelea kuwaletea maendeleo ,ikiwa ni utekelezaji wa  ahadi ya Rais Dk. Hussein  Mwinyi wakati wa kampeni zake  .
Hayo yalisemwa katika kikao na Ujumbe wa Shirika la Ufadhili wa Misaada ya Fedha kutoka Uingereza (UK FINANCE EXPORT ) ambao wameambatana na Kampuni ya Ujenzi ya Propav kilichofanyika jana  jijini hapa ,chenye lengo la kujadiliana namna bora ambayo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaweza kushirikiana na Taasisi ya UKF Katika kuleta maendeleo katika mbalimbali .
Akizungumza Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais  Fedha Fedha na Mipango Jamal Kassim Ali , alisema Serikali imejipanga kuhakikisha inatekeleza ahadi zote zilizoahidiwa,na kuleta maendeleo katika sekta za usafirishaji na sekta nyingine za kijamii visiwani Zanzibar   .
Alizitaja Sekta nyengine ni uboreshaji na uendelezaji wa uwanja wa ndege kisiwani Pemba,pamoja na ujenzi wa hospitali ya Binguni,na ujenzi wa Bandari ya Uvuvi huko Mangapwani.
Alianisha barabra zitakazo tekelezwa chini ya ufadhili wa mradi huo ,Chakechake  mkoani ,Kisauni Fumba ,Tunguu Makunduchi na pamoja na uendelezaji wa Uwanja wa ndege wa Pemba ambapo miradi hii tayari serikali imeingia katika makubaliano na Kampuni ya Propav kwa ajili ya utekelezaji wake.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa UKF Kanda ya Afrika Mashariki Isaac Kahara alisema mikakati na mipango yao katika kusaidia maendeleo ya jamii ya watu wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.