Mhe. Waziri aeleza dhamira ya Kukusanya Mapato kwa mfumo mpya wa kielektroniki

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe. Jamal Kassim amesema Serikali inakadiriya kukusanya Mapato na kufanya Matumizi ya TZS 1,845.6 bilioni 2021/2022 na kueleza dhamira ya Serikali ni kuanza kukusanya Mapato kwa kutumia Mfumo mpya wa kielektroniki “ZANMALIPO” ili kurahisisha ukusanyaji wa mapato hayo.

Mheshimiwa Jamal ameahidi kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 10 kwa utaratibu wa “duty remission “ malighafi yenye code HS 5407.71.00 na kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 10 hadi asilimia 0 kwa mwaka malighafi code HS 5402.33.00 zote zinazotumika kutengenezea nguo.

Aidha Mhe. Jamal amesema Serikali inapendekeza kufanya marekebisho ya sheria ya usimamizi wa kodi Namba 7 ya mwaka 2009 kwa kuweka adhabu TZS 2milioni kwa kila muamala kwa wafanyabiashara ambao hawatoi risiti.

Mkakati wa Serikali ni kudhamiria kusimamia utekelezaji wa Mipango na Bajeti inayoakisi Uchumi wa Bluu kwa Maendeleo ya Zanzibar na watu wake.
Mheshimiwa Jamal ameeleza hayo na mengine mengi alipokuwa akiwasilisha Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2021- 2022