Mhe. Waziri aendelea na Ziara yake kujitambulisha Taasisi ya TIRA – Zanzibar

Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe. Jamal Kassim Ali ameendelea na Ziara zake za kujitambulisha katika Taasisi zilizochini ya Wizara yake. Mhe. Jamal ametembelea Taasisi ya TIRA iliyopo kilimani Zanzibar. Mhe. Waziri ameutaka Uongozi wa TIRA kufanya utafiti wa kuweza kujua kama kuna wananchi wanaohitaji bima za moto ili kuweza kuokoa majanga yanayowakali wananchi.

Mhe. Jamal alisema ma “broker” wa bima kuepuka udanganyifu kwani mara huwa wanatoa stika za bima lakini kiukweli huwa hazina bima za kampuni husika, pia Mhe. Jamal aliuomba Uongozi wa TIRA kujiunga na Mtandao wa Serikali katika kuzisajili bima za magari au majengo na kuushauri Uongozi huo kuanzisha huduma za bima za kiislamu.