Mhe. Waziri afanya mkutano na wafanya Biashara tofauti katika ukumbi wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB).

Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe. Jamal Kassim Ali ameahidi kuboresha Mazingira ya Wafanyabiashara ili waweze kufanya biashara kwa ufanisi zaidi na kuweza kujipatia tija kwao na kwa Taifa. Mhe Jamal amesema Wafanyabiashara ni kichocheo kikubwa cha kukuza Uchumi wa nchi na kuipatia Serikali Mapato yanayopelekea kuleta Maendeleo ya Nchi yetu.

Mhe. Waziri ameyasema hayo leo alipozungumza na Wafanyabishara mbalimbali wa Zanzibar kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB).