Mhe. Waziri akutana na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia.

Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mheshimiwa Jamal Kassim Ali amekutana na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dr. Ramadhan Kitwana Dau. Mheshimiwa Jamal na Balozi Dr. Ramadhan wamezungumzia juu ya fursa za Uwekezaji zinazopatikana Nchini Tanzania Zanzibar kwa wananchi wa Malaysia. Mheshimiwa Jamal amemuahidi Balozi Ramadhan kwamba watazitumia fursa hizo ambazo watu wa Malaysia wanazihitaji na kuja kuekeza Zanzibar. Aidha Mhe. Jamal amesema kuwa Zanzibar kuna vivutio vingi vya Uwekezaji ambavyo ikiwemo jina lenyewe la nchi yetu pia amani na utulivu wa nchi yetu, pamoja na Sera nzuri za kiuwekezaji, ambapo Mhe. Jamal amesema uwekezaji huo utapelekea kukuza Uchumi na kutuletea Maendeleo ndani ya nchi yetu.