Mhe. Waziri akutana na kufanya mazungumzo na Saud Fund

Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mheshimiwa Jamal Kassim Ali leo amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Saud Fund wenye nia ya kuisaidia Zanzibar katika kuboresha Miundombinu ya Barabara za ndani na ukarabati wa ujenzi wa Hospitali ya Mnazi Mmmoja. Mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Afisi ya Rais Fedha na Mipango Vuga- Mjini Zanzibar.