Mhe. Waziri akutana na Viongozi mbalimbali wa kampuni za Bima Wizarani kwake – Zanzibar

Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe. Jamali Kassim Ali amekutana na Viongozi wa Kampuni za Bima Tanzania hapo Ofisini kwake Vuga.

Mhe. Jamal Kassim amewataka Viongozi wa kampuni za Bima kutoa elimu ya Bima zote kwa Jamii ili wananchi waweze kujikatia bima hizo. Aidha, Mhe. Waziri amesema wananchi walio wengi hawaelewi gharama za bima ya majanga ya moto, elimu hiyo itawasaidia wananchi kukata bima ya moto na kujinusuru na majanga.