Mhe. Waziri amefanya Ziara ya kutembelea Tume ya Pamoja ya Fedha iliyopo Kinazini

Mhe. Waziri Jamal Kassim Ali amefanya ziara ya kutembelea Tume ya Pamoja ya Fedha iliyopo kinazini na Kuonana na Katibu Msaidizi ndg. Wadi Haji Ali Pamoja na kuonana na watendaji wenginge wa Tume hiyo. Aidha, Mhe. Jamali alipokea changamoto za tume hiyo pia alifurahishwa na utendaji kazi zao, namna wanavyoishauri Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye Masuala ya Mfuko huo yanayohusu mambo ya kiuchumi, mahusiano ya kifedha za Muungano juu ya kugawana kwa mapato ya serikali zote mbili.