Mhe. Waziri aongea na uongozi wa Benki ya Watu wa Z’bar (PBZ) – Pemba

Mhe. Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe. Jamal Kassim Ali Leo asubuhi aliushauri uongozi wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ tawi la Mtemani Wete Pemba kufikiria mfumo mzuri wa biashara kwa wakulima wa karafuu ili kuweza kuinua uchumi wa nchi. Mhe. Jamal Alisema iwapo mtawasaidia wakulima wa karafuu kwa uchumaji, ukaushaji kwa kuwawezesha kifedhaa Waziri Jamal alisema mtu akijua hasa kama amedhaminiwa na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) itakuwa rahisi mfanyabiashara huyo au mkulima wa karafuu baada ya mavuno kuja kuziweka pesa zake ndani ya Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).
Aidha, Waziri Jamal aliutaka Uongozi wa PBZ kumfikiria mteja wake ambae ni shirika la ZSTC linawekeza fedhaa zake katika benki ya PBZ ikiwa Shirika hilo itazichukuwa fedha zake na kwenda kununua karafuu kwa wakulima au kwafanyabiashara ambao hawana akaunti katika benki ya PBZ Mhe. WEaziri aliuliza hawaoni kwamba fedha hizo