Mhe. Waziri azungumza na balozi wa Uarabuni (UAE)

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango, Jamal Kassim Ali, amekutana na Balozi wa Falme za Kiarabu, Khalifa Abdulrahman Almarzooqi, na kuzungumza naye kuhusu maendeleo na utelezaji wa miradi mbalimbali Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari,katika Ofisi za Serikali ya Mapinduzi (SMZ), Dar es Salaam, baada ya mazungumo yao, Waziri alisema wamezungumza mambo mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Hospitali ya wete, Pemba.
Pia alisema eneo la pili la mazungumzo yao ni kuhusu uwezeshaji wananchi kiuchumi, hususan wanawake na vijana, fedha ambazo ni Dola milioni 10, zilipangwa na serikali kuelekezwa katika taasisi ya Smida.
Alisema kuna changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika kutekeleza miradi, hivyo wameomba namna ya kusaidiwa kutekeleza miradi ambayo iko mingi ambayo haijakamilika.
Alisema katika mazungumzo hayo balozi huyo, aliweka ahadi ya kushirikiana na Zanzibar katika kuwapatia fursa za kimasomo za muda mrefu na mafunzo ya muda mfupi.
Waziri alimshukuru balozi huyo kwa ushirikiano aliyounyesha kwa zanzibar na ameonyesha utayari mkubwa binafsi atahakikisha mambo yote atayasimamia na hatimaye kuleta matunda nchini Zanzibar.