Mhe. Waziri azungumza na Wakaguzi wa ndani.

Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mheshimiwa Jamal Kassim Ali amesema Serikali haitomvumilia Mkaguzi wa Ndani yeyote atakaeshindwa kusimamia vizuri Miradi iliyo chini ya Wizara anayoifanyia kazi. Mhe. Jamal amesema Miradi mingi inakuwa chini ya viwango na kupelekea fedha za Serikali kupotea.Mheshimiwa Waziri amewataka wakaguzi wa Ndani kuanza kazi ya kukagua Miradi iliyo chini ya Wizara zao ili kubaini mapungufu ya Miradi hiyo.Mhe. Jamal amewataka wakaguzi hao kuwa wazalendo zaidi juu ya kazi yao na aliwataka wakaguzi hao kujitathmini na kufanyakazi kwa ufanisi ili kuisaidia Serikali katika kutatua matatizo na changamoto za Miradi.Hata hivyo Mhe. Jamal ameahidi kuunda timu maalum itakayochunguza matumizi ya fedha za Miradi miwili ya Serikali ambayo ni Mradi wa barabara inafadhiliwa na Soudi Fund, BADEA pamoja na Mradi wa E-Government. Mheshimiwa Jamal ameyasema hayo hapo Ofisini Vuga kwake alipozungumza na Wakaguzi wa Ndani wa Serikali.