Mhe. Waziri katika majumuisho ya Ziara yake ya siku mbili Pemba

Mhe. Jamal Kassim Ali katika majumuisho ya Ziara yake ya siku mbili aliyoifanya Pemba aliwataka Wafanya kazi wote waliochini ya Wizara yake kila mmoja kufika kazini mapema na kuondoka kwa muda uliowekwa na kufuata kanuni za Utumishi Serikalini. Mhe. Waziri alisisitiza kila mmoja afanyekazi kulingana na majukumu yake ya kazi aliwasisitiza wafanyakazi hao kuweka mpango mkakati na kujiwekea vipimo vya kazi ili kufikia malengo yaliyo pangwa katika ilani ya Uchaguzi, kuangalia Ahadi za Mhe. Rais wa Zanzibar alizozitoa wakati wa Kampeni za Uchaguzi na mambo kumi na tatu ambayo aliwataka mawaziri wayafanyie kazi wakati wa kuwaapisha Mawaziri. Aidha, Mhe. Jamal aliwasisitiza wafanyakazi hao kuwa na nidhamu kwani suala la nidhamu kazini ni muhimu katika kufanikisha malengo ya kazi.  Mhe. Waziri aliwaahidi Viongozi na Wafanyakazi hao kuwa atarudi tena