Mhe. Waziri kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Wizara ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kiuchumi ya Ujerumani

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMEDHAMIRIA KUWALETEA MAENDELEO YA HARAKA WANANCHI WAKE KUPITIA SEKTA MBALI MBALI. Hayo yamedhihirika wakati Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe Jamal Kassim Ali alipofanya mazungumzo na wawakilishi wa Wizara ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kiuchumi ya Ujerumani juu ya kuisaidia Serikali katika za Maji,Michezo na Mazingira Waziri Jamal amewahakikishia wawakilishi hao kuwa serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Mh Rais Dr Husein Ali Mwinyi inayo nia ya dhati ya kuhakikisha inasogeza huduma zote muhimu karibu na makaazi ya wananchi, aidha Waziri Jamal amewahakikishia wawakilishi hao kuwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo tayari kupokea kushirikiana nao ili kuweza kuleta maendeleo ya haraka kwa wananchi Nao wawakilishi hao wamemuahidi Waziri huyo kuwa wapo tayari kuisaidia Serikali katika sekta muhimu ya maji,michezo pamoja na mazingira