Mhe. Waziri kufanya ziara ya kuzitembelea Ofisi za Afisa Mdhamini Pemba

Mhe. Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe. Jamal Kassim Ali amewasili kisiwani Pemba na kufanya ziara ya kuzitembelea Ofisi za Afisa Mdhamini Pemba iliyopo Gombani kwa lengo la kujitambulisha. Afisi hizo zilizotembelewa ni zile zilizochini ya Wizara yake pia alipata wasaa wa kuonana na watendaji na wafanyakazi wa Wizara hiyo ili kujionea maendeleo na Changamoto zinazowakabili wafanyakazi hao. Aidha, Afisa Mdhamini wa Wizara hiyo Nd.Ibrahim Saleh Juma alimueleza Mhe. Waziri kuwa kwa sasa katika jengo lao wanakabiliwa na changamoto ya “lift” kwani wanapokuja wazee kufuatilia mafao yao inakuwa usumbufu kidogo kwani wazee hao wanakuwa hawawezi kupanda juu na hulazimika wafanyakazi kushuka chini ili kuwahudumia wazee hao.