Mheshimiwa Dkt. Saada Mkuya Salum akifunga Kongamano la nne la kumbukizi ya Rais wa Kwanza na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume

Waziri wa Nchi Ofisi Ya Rais, Fedha na Mipango Mheshimiwa Dkt. Saada Mkuya Salum akifunga Kongamano la nne la kumbukizi ya Rais wa Kwanza na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume. Mheshimiwa Dkt. Saada amesema suala la kuwakumbuka viongozi waliopita ni Jambo muhimu sana na liwe linaendelea ili vijana wapate kuelewa vipi viongozi waliotangulia walitoa michango yao kwa maendeleo ya taifa. Mheshimiwa Saada ameyasema hayo alipokuwa akilifunga kongamano hilo la mchango wa hayati karume katika maendeleo ya elimu na Uchumi wa Zanzibar. Aidha, Dkt. Saada amesema tukiwa tunamzungumzi Hayari Karume huwezi kuacha kuzungumzia maendeleo ya jamii pamoja na kukua kwa uchumi wa Zanzibar kwani Hayati karume alianzisha viwanda vidogovidogo ikiwemo kiwanda cha ZAFICO na kuanzisha kwa benki ya watu wa Zanzibar, pia alivyoambiwa makaazi bora na elimu bure Zanzbar. Mheshimiwa Dkt. Saada alipokea changamoto na kusema sera ya elimu inafanyiwa kazi