Mheshimiwa Dkt. Saada Mkuya Salum kufanya Ziara Mjini

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Mheshimiwa Dkt. Saada Mkuya Salum akiongozana na Kamishna wa ZRB Ndg. Yusuph Juma Mwenda wamefanya Ziara ya kutembelea maduka mengi katika maeneo ya darajani, michenzani mall, kilimani, chukwani na kumalizia kiembe samaki. Mheshiwa wametembelea baadhi ya maduka ya wafanya biashara ili kuangalia matumizi ya VFMS na utowaji wa risiti za kielektroniki. Mhe. Dkt. Saada amebaini kuwa karibia maduka yote wafanyabiashara hawatoi risiti za kielektroniki na wanunuzi wananchi hawana muamko wa kudai risiti za kielektroniki. Aidha, Mheshimiwa Saada amesema Serikali itachukuwa hatua kali kwa wale ambao wanakaidi haya maagizo ya kutoa risiti na wale ambao wafanyabiashara wanaweka bei mbili. Kwani wapo wafanyabiadhara huwa wanawambia wananchi ukitaka risiti bei hii na bila risiti utalipa bei hii. Dkt. Saada amesema kutokutoa na kudai risiti za kielektroniki ni kosa kisheria. Mheshimiwa amewataka wafanyabiashara wote walokuwa na changamoto ya utumiaji wa VFMS wafike ZRB kwa kutatuliwa changamoto hizo. Mhe. Dkt. Saada ameiagiza ZRB kuhakikisha wale wote wafanyabiashara ambao wanaotumia mifumo isiyokuwa ya ZRB mifumo hiyo iungwanishwe haraka iwezekanavyo na mifumo ya ZRB. Ziara hiyo aliifanya asubuhi ya tarehe 04/06/2022 na kumalizia magharibi yake.