Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum aonana na Benki ya Dunia

Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum leo amekutana na Ujumbe kutoka Benki ya Dunia ukiongozwa na Bi Yaa Oppong Mkuu wa kitengo cha Maendeleo endelevu anaeshughulikia masuala ya upande wa Afrika ikiwemo nchi ya Tanzania na kuzungumzia kuhusu masuala ya maendeleo kwa upande wa Wanawake na Walemavu kwa upande wa Zanzibar. Benki ya dunia inaandaa Miradi ambayo itazingatia masuala ya uwezeshaji kwa wanawake, hii imetokana na ziara za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan kuona kwamba uwezeshaji wa wanawake unafanyiwa kazi. Mazungumzo hayo yamelenga juu ya Miradi ambayo Benki ya dunia itakavyoweza kuisaidia Zanzibar kwa kuandaa miradi ya kimaendeleo ili kuwawezesha wanawake kiuchumi. Miradi hiyo itakuwa katika pande zote za Muungano wa Tanzania . Ujumbe huu upo Zanzibar ukiangalia maeneo ya kuekeza mradi huo. Tayari ujumbe huo umeshatembelea Wizara husika ya Jinsia Wanawake na Watoto pamoja na ofisi ya Walemavu- OMKR na kufanya mazungumzo ya awali na leo Ujumbe huo umeonana na Mhe. Dkt. Saada mazungumzo yao yamelenga zaid jinsi ya miradi itakavyoanzishwa na kuwasaidia wanawake kiuchumi ili kupunguza umaskini, kwani maeneo mengi hususan ya kiuchumi wanawake wapo nyuma kuliko wanaume. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ya Rais Fedha na Mipango- Vuga.