SERIKALI YAFANYA MAZUNGUMZO NA BENKI YA EXIM YA INDIA

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefanya mazungunzo na Mkurugenzi Mkuu wa Benk ya Exim ya India Ndg. Gaurav Singh Bhandari. Mazungumzo hayo yameongozwa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Ndg. Juma Malik Akili ambapo Benk ya Exim ya India inatarajiwa kuipatia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar jumla ya Dola za Marekani 92.18 Milioni, ambazo fedha hizo zitatumika kugharamia Mradi wa Uhuishaji na Uimarishaji wa mfumo wa Maji Zanzibar. (REHABILITATION AND IMPROVEMENT of Water Supply System in Zanzibar – RIWSSZ).Katibu Juma amesema Lengo la Mradi ni kurahisisha upatikanaji wa Maji safi na Salama Nchini.Mazungumzo hayo yalijadili changamoto ya Misamaha ya Kodi ambapo Serikali imeahidi italifanyia kazi suala hilo ili kuondoa usumbufu uliojitiokeza.
Mradi huo unatarajiwa kuchimba visima 64 vyenye uwezo wa kuzalisha jumla ya lita 7,632,000 kwa saa, Matangi 17 yatakajengwa Mradi huo pia utasaidia Mabomba yote 482.984 visima hivyo vinatarajiwa kuchimbwa katika maeneo ya Wilaya Magharibi A, Wilaya ya Magharibi B, Wilaya ya Kati na Wilaya ya Kaskazini B.