Waziri Jamal Ameizindua bodi ya Shirika la bima Zanzibar

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe. Jamal kassim Ali amelitaka Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) kuwa wabinifu katika kutafuta wateja hasa nje ya Tanzania ili kuendana na ushindani wa kibiashara uliopo sasa. Kwani hatua hiyo itaiwezesha shirika hilo kupiga hatua ya uzalishaji zaid.
Mheshimiwa Jamal amesema kwavile shirika hilo ni lamwanzo kusogeza huduma zake Tanzania bara na tayari wameshajulikana maeneo mengi ndani ya Mikoa ya Tanzania, hivyo hakuna sababu ya kuweza kukaaa katika sehemu moja na wabuni biashara itakayo endana na mahitaji ya watu katika pande za Afrika Mashariki.
 Mhe.Jamal amewasihi watendaji wa Shirika  hilo kusimamia mifumo yandani Ili kukidhi mahitaji ya wateja katika maeneo ya utendaji  wa kazi zao. Na kuwaagiza waanzishe Bima ya Afya nchini. Waziri Jamal ameyasema hayo alipokuwa akiizindua bodi ya Shirika la Bima Zanzibar hapo Mperani.
Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika  la Bima Zanzibar Ndo. Ramadhani Mwalim Khamis amesema tayari shirika hilo limeshaanzisha mikakati mbali ya kuanzisha bima mbali ikiwemo bima ya watalii na wavuvi ilikuwafikia wateja wengii.