Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango kufanya majadiliano baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Uongozi wa OPEC/OFID

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeushukuru Uongozi wa Mfuko wa Maendeleo wa Nchi zinazozalisha Mafuta kwa wingi Duniani (OFID) kwa kuendelea kuisaidia Zanzibar katika sekta mbali mbali zikiwemo Elimu, Afya na Miundombinu. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Mhe.

Dkt Saada Mkuya Salum ameyasema hayo wakati walipokutana na kufanya majadiliano ya pamoja baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Uongozi wa OPEC/OFID Dkt Sada aliongozana Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Leila Mohammed Mussa, Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Mhe. Dkt Khalid Salum Mohammed, Waziri wa Afya Mhe. Nassor Ahmed Mazrui pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Mhe. Ali Suleiman Ameir (Mrembo) Aidha, Mawaziri hao wametoa shukrani zao za dhati Kwa Uongozi wa Mfuko wa OPEC Kwa kuisaidia Zanzibar katika Miradi ya Elimu ikiwemo ujenzi wa skuli ya Chumbuni na Skuli ya Dkt. Ali Mohammed Shein sambamba na kusaidia sekta ya Afya na Sekta ya Miundombinu ikiwemo ujenzi wa barabara tatu ambazo ni barabara ya kitope kidimni, kitundu ndagaa na barabara ya machui barabara hizo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kuinua uchumi wa Zanzibar na kupunguza Umaskini nchini. Mawaziri hao wameuomba Uongozi huo uendeleze jitihada zake za kuisaidia Zanzibar katika ujenzi Miradi ya barabara, Utanuzi wa uwanja wa Ndege Nungwi pamoja na kusaidia kujenga jengo la maabara ya kisasa ya utafiti wa afya ya binadamu. Baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa skuli mbili za Chumbuni Sekondari na Skuli ya Dkt. Ali Mohammed Shein zilizojengwa kwa ufadhili wa OPEC/OFID Mkurugenzi Mkuu wa OPEC ameipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Kwa matumizi mazuri ya Fedha za Miradi zilizotolewa na OPEC FUND.

Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa OPEC Dkt Alkhalifa Abdulhamid Saleh ameahidi kuendelea kuisaidia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika Miradi ya Utanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Terminal 2, Miundombinu ya barabara na sekta ya Afya.