Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- fedha na Mipango Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum ametiliana saini na Balozi wa Uingereza Mhe. David Concar pamoja na Citi Benki ya Tanzania Nd. Geofrey Mchangila akiiwakilisha Citi Benki ya London.
Mkataba huyo unakadiriwa kutumika jumla ya Uro Milioni 181kwa upande wa ujenzi wa Airport Pemba na kwa upande wa Ujenzi wa Miundombinu ya Barabara inakadiriwa kutumika jumla ya Uro Milioni 230 zitakazo tumika kwa kujengwa barabara 3.
Barabara zenyewe ni barabara ya ChakeChake hadi Mkoani Pemba, kisauni hadi Fumba na barabara ya Tunguu hadi Makunduchi.
Waziri saada Mkuya amesema Ujenzi wa barabara hizo pamoja na ujenzi wa Airport itaimarisha utalii Nchini.