Naibu Waziri Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Hamad Omar amefungua Warsha ya Uelewa juu ya Mfumo wa ZanSDI kwa wafanyabiashara wa Zanzibar kupitia Mradi wa BIG-Z.
Akifungua warsha hiyo amesema ni sehemu ya mfululizo wa programu endelevu za mafunzo zinazolenga kuwasaidia wafanyabiashara wa ndani.
Amesema hatua hii itasaidia kuimarisha ufanyaji wa maamuzi sahihi na kukuza uchumi wa biashara katika nchi yetu ya Zanzibar.