Waziri wa Nchi – Afisi ya Rais- Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum leo tarehe 07/08/2023 amezindua tawi la PBZ liliopo Airport na Tunguu.
Dkt. Saada amesema amefurahishwa na hatua zinazochukuliwa na PBZ za kuwasogezea karibu huduma za kifedha wananchi.
Dkt. Saada amesema kituo cha Airport ni kituo pekee ambacho kinatoa huduma zote za kibenki kwa masaa 24 na siku zote za wiki.
Dkt. Saada amefurahishwa kwakua PBZ inafanya mabadiliko makubwa ya kimaendeleo.
Aidha Dkt. Saada amesema kuwa PBZ inafanya vizuri sana na inaelekea kufikia maono ya Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi ni kuona maendeleo yapatikana Nchi ikiwemo kuwasogezea karibu huduma za kifedha na kupatikana kwa urahisi Nchini.
Dkt. Saada amesema kuongezeka kwa watumiaji wa huduma za kifedha hii inatokana na dira ya Maendeleo ya 2050, ilani ya CCM ,Sera ya fedha pamoja na Sera ya Uwekezaji Nchini.
Nae Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Muusin S. Masoud amesema PBZ inalengo la kuwasogezea wananchi huduma bora za kibenki pia inatoa gawio kwa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na matarajio yao kufungua matawi ndani ya Zanziba, Tanzania na Afrika kwa ujumla.






Imeandaliwa na
Kitengo cha habari na Uhusiano
Ofisi ya Rais- Fedha na Mipango