Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum amesema amefurahishwa na kuona PBZ kuchangamkia fursa muhimu na kuona PBZ anayoitaka ndo anayoiona sasa kwa kuharakisha kwa utiaji Saini wa Cashless.
Waziri Dkt. Saada ameyasema hayo huko Golden tulip wakati akiwa mgeni rasmi katika hafla ya uwekaji saini kwa niaba ya SMZ, saini hiyo imewekwa baina ya PBZ Bank ikishirikiana na E – Government na ACU ( Asia Currency Unity).
Waziri Dkt. Saada amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inataka kuingia katika mfumo wa Cashless katika nyanja ya matumizi kwa Zanzibar nzima.
PBZ BANK kwakushirikiana na E-Government na ACU (Asia Currency Unity) wamekuja na mkakati wa pamoja ya kuhakikisha wanautekeleza kivitendo mfumo huo wa Cashless baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Mhe. Dkt. Saada amesema mfumo huo utapunguza ukamataji wa cash katika matumizi ya Serikali na kusisitiza lazima kuwepo na matumizi ya kidigitali Nchi nzima.
Aidha, Dkt. Saada aliwataka wananchi waweze kuyakubali mabadiliko hayo ili Serikali iweze kuendelea kukusanya mapato yake na kuweza kufanya matumizi kwa kutumia mfuo huo wa Cashless Nchini.