Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais – Fedha na Mipango Mhe. Dkt Saada Mkuya Salum leo Mei 29,2023 amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), ujumbe huo umeongozwa na Ng. Christine Meacsi
Mazungumzo hayo yenye lengo la kuipatia Zanzibar Fedha kupitia Bondi za Kiislam (Sukuk bond) yamefanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Ofisi ya Rais- Fedha na Mipango Vuga, Mjini Zanzibar
Mhe. Waziri Dkt. Saada Mkuya ameeleza kuwa Zanzibar inatarajia kufanya Miradi ya Kimkakati ikiwemo ujenzi wa Bandari ya Mangapwani, Ujenzi wa Terminal 4 na kujenga Barabara za juu (Fly Over), hivyo Kuna haja ya kuharakisha Sukuk bond ili fedha zipatikane kwa haraka Kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo.
Nae Ndg. Christine Meacsi kutoka UNDP ameeleza kuwa UNDP imekuja na mpango wa Bondi za Kiislam (Sukuk bond) ili kuzisaidia Nchi za Kiislam kupata Mikopo Kwa njia rahisi kutoka UNDP
Aidha, ameendelea kueleza kuwa UNDP wana mashirikiano ya karibu na Benki ya Maendeleo ya Kiislam (IDB), hivyo itasaidia kuboresha Sukuk bond.