WhatsApp Image 2023-05-12 at 1.32.56 PM (1)

Waziri amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway Nchini Tanzania Mhe. Balozi Elisabeth Jacobsen.

Waziri wa Nchi- Ofisi ya Rais – Fedha na Mipngo Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum leo Mei 11, 2023 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Norway Nchini Tanzania Mhe. Balozi Elisabeth Jacobsen.

Balozi Elisabeth ameeleza kuwa amekuja kumuaga Mhe.Waziri baada ya muda wake kumalizika.

Mhe. Waziri Dkt. Saada Mkuya ameishukuru Serikali ya Norway kwa ushirikiano na Uhusiano mzuri uliopo baina ya Nchi hizi mbili.

Waziri Dkt. Saada amemueleza Mhe. Balozi Elisabeth kuwa Norway imekuwa ikishirikiana Kwa muda mrefu na Tanzania na imeisaidia Zanzibar katika Miradi mbali mbali ikiwemo Mradi wa kutoa Umeme Tanga hadi Pemba, Kebo za marini kutoka Dar mpaka Zanzibar pamoja na Kusaidia ujenzi wa hospitali ya afya ya akili kidogo chekundu.

Mhe. Dkt Saada ameeleza kuwa Zanzibar itaendelea kumpa ushirikiano Balozi wa Norway atakae kuja Nchini Tanzania na kuendeleza kukuza mashirikiano yaliopo

Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Ofisi ya Rais Fedha na Mipango
11 Mei, 2023

Tags: No tags

Comments are closed.