Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum leo Mei 03, 2023 amepokea ujumbe wa Viongozi 70 kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania (National Defense College)
Baada ya mapokezi hayo, Mhe. Waziri Saada ameongoza mkutano katika Ukumbi Shirika la bima la Zanzibar
Aidha, Viongozi hao wa kijeshi walipata fursa ya kusikiliza uwasiliahwaji wa hali ya Uchumi wa Zanzibar pamoja na vipaumbele vyake kupitia Dira ya Maendeleo ya 2050
Viongozi hao wa kijeshi wameeleza kuwa wamejifunza mambo muhimu sana Zanzibar hasa Uchumi na Utalii kwani, Uchumi, kilimo na Utalii ni Usalama wa Taifa bila ya Uchumi imara vitendo vya kihalifu huongezeka
Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Ofisi ya Rais Fedha na Mipango
03 Mei 2023