0E6A7570

MHE. WAZIRI AKUTANA NA WAFANYAKAZI WA OFISI YA RAIS, FEDHA NA MIPANGO ZANZIBAR

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Mhe. Dkt Saada Mkuya Salum Leo Agosti 27 amekutana na Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake

Mkutano huo, umefanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdulwakil Kikwajuni, Mjini Zanzibar

Katika Mkutano huo, Mhe. Waziri amewapongeza Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Kwa kuchangia mafanikio ya Wizara pamoja na Bajeti ya Wizara na Serikali ya Mwaka 2023/2024

Aidha, Mhe. Dkt Saada Mkuya Salum ameeleza kuwa Kuna haja ya kuanzisha Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais Fedha na Mipango lenye muundo wa Mwenyekiti, Katibu na Wajumbe Kwa lengo la kufuatilia na kutatua changamoto za Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango

Katika nasaha zake Mhe. Waziri amewataka Wafanyakazi kutunza vifaa vya Ofisi, kujiepusha na rushwa na ubadhilifu wa mali za Umma pamoja na kujiepusha kutumia intaneti ya Ofisi Kwa masuala binafsi

Nae, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Dkt Juma Malik Akil amewataka Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango kufanya kazi Kwa bidii, uadilifu na mashirikiano

Pamoja na mambo mengine, Wafanyakazi hao wamepata fursa ya kuulzia masuali, kutoa maoni na mapendekezo mbalimbali na Viongozi wa Ofisi ya Rais Fedha na Mipango wakapata fursa za kutoa ufafanuzi wa masuali yaliyoulizwa

Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango
27 Agosti, 2023

Tags: No tags

Comments are closed.