Divisheni hii inahusika na masuala ya utawala, uendeshaji na usimamizi wa shughuli za kila siku za Ofisi. Divisheni hii inaongozwa na Mkuu wa Divisheni.
Majukumu ya Divisheni ya Uendeshaji
- Kuweka kumbukumbu za matukio muhimu katika sehemu ya kazi;
- Kusaidia kusimamia nidhamu ya wafanyakazi;
- Kusimamia matumizi na matunzo ya vifaa vya Ofisi ikiwemo vyombo vya usafiri, magari, mitambo, samani, vifaa vya kuandikia na vifaa vya mawasiliano;
- Kusimamia majengo na mali za Ofisi;
- Kusimamia shughuli za kiufundi na uendeshaji wa maghala ya Ofisi;