Divisheni hii inahusika na masuala ya utawala, uendeshaji na usimamizi wa shughuli za kila siku za Ofisi. Divisheni hii inaongozwa na Mkuu wa Divisheni.
Majukumu ya Divisheni ya Uendeshaji
Kuweka kumbukumbu za matukio muhimu katika sehemu ya kazi;
Kusaidia kusimamia nidhamu ya wafanyakazi;
Kusimamia matumizi na matunzo ya vifaa vya Ofisi ikiwemo vyombo vya usafiri, magari, mitambo, samani, vifaa vya kuandikia na vifaa vya mawasiliano;
Kusimamia majengo na mali za Ofisi;
Kusimamia shughuli za kiufundi na uendeshaji wa maghala ya Ofisi;