- Kutafuta Kumbukumbu/Nyaraka/Mafaili yanayohitajiwa na watumishi wa Ofisi
- Kupokea na kudhibiti na kutunza kumbukumbu za Ofisi
- Kuchambua, kuorodhesha na kupanga Kumbukumbu/Nyaraka katika makundi kulingana na mada husika (classification and boxing) kwa ajili ya matumizi ya Ofisi;
- Kuweka/kupanga Kumbukumbu/Nyaraka katika reki (file racks/cabinets) katika Masjala na vyumba vya kuhifadhi kumbukumbu tuli za Ofisi
- Kuweka na kutunza kumbukumbu (barua, nyaraka n.k) katika Mafaili;
- Kushughulikia maombi ya Kumbukumbu/Nyaraka kutoka kwa maafisa mbali mbali na Taasisi za Serikali;
- Kuhifadhi Majalada yaliyofungwa kwa Kumbukumbu za baadae.